MIBURO Anne, msichana mwenye umri wa miaka 17 
aliripotiwa katika gazeti hili Mei 27, mwaka huu ikiwa na kichwa cha 
habari ‘NINASUBIRI  MUNGU AICHUKUE ROHO YANGU’, amefariki dunia wiki 
iliyopita akiwa njiani kurejea nyumbani kwao, nchini Burundi.
Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akisumbuliwa na uvimbe mwilini, 
alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako ugonjwa 
wake ulishindwa kutibika.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, mwanafunzi huyo alianza kuumwa tokea 
akiwa kidato cha pili, hali iliyomlazimu kuacha kwenda shule ili 
kufuatilia matibabu, ambayo yalimfikisha katika Hospitali ya Taifa 
Muhimbili.
Kaka wa marehemu aliyetambuliwa kwa jina moja la Albert alisema mdogo wake alipoteza maisha wakiwa mpakani mwa nchi hizi mbili na kwamba alimhangaikia sana ili aweze kupona licha ya uwezo wake mdogo kifedha
 


 
 
No comments:
Post a Comment