Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema serikali yake itaendelea
kupambana vikali na wahalifu pamoja na magaidi na kuwataka polisi
kumpiga risasi mara moja mtu yeyote anayeonekana kutishia usalama wa
taifa. Rais Kagame amesema kuna taarifa zinazoonyesha kuwa, kundi la
FDLR linalotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994
linajipanga upya na kwa mantiki hiyo amevitaka vyombo vya usalama kuwa
macho.
Huku hayo yakijiri, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Bi. Louise Mushikiwabo, amekanusha vikali madai ya Marekani kwamba serikali ya Kigali inawabana waandishi wa habari pamoja na kukiuka haki za kujieleza za raia. Waziri Mushikiwabo amesema Rwanda ina uhuru wa kujiendeshea mambo yake na wala haihitaji ushauri wa Washington. Siku mbili zilizopita, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa taarifa inayoituhumu Rwanda kuwa inakiuka haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuvibana vyombo vya habari na kumtaka Rais Kagame kuheshimu sheria za kimataifa zinazolinda uhuru wa kujieleza wa raia kote duniani.

No comments:
Post a Comment