Mtuhumiwa huyo, William Sebastian (21), mkazi wa Kijiji cha Mlezi alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo, Faustine Kishenyi.
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Samwel Onyango aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 4 mwaka huu saa 9 alasiri huko Mlezi, Ukerewe.
Katika hati ya mashitaka imeelezwa kuwa mshitakiwa huyo alikutwa akitenda kosa hilo katika banda la mbuzi nyumbani kwao na mmoja wa wanafamilia.

Katika maelezo hayo, Onyango alisema mwanafamilia huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mlezi, baada ya kushuhudia tukio hilo alikwenda kutoa taarifa kwa baba yao, Maxmilian Stephan aliyefika na kumkuta mtuhumiwa akiendelea `kuhangaika’ na mbuzi huyo.
No comments:
Post a Comment