Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewashauri viongozi wazee na waliokaa madarakani muda mrefu kuacha kung’ang’ania madaraka.
Aliongeza: “Haiwezekani mzee ukakaa kundi moja na kijana wako
aliyetahiriwa juzi, kwani kwa kawaida, kijana akitahiriwa hupandishwa
daraja na kukaa kundi la wakubwa, hapo wewe baba yake hata kama una
miaka 40, unahamishwa na kuingia kundi la wazee.”
Januari 14, 2010, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliwashauri wazee
watumie busara kupima uamuzi wa kugombea tena nafasi za ubunge kwenye
uchaguzi mkuu. Pinda alitoa rai hiyo alipokuwa akijibu maswali ya
wahariri katika mkutano alioitisha kujibu maswali yao jijini Dar es
Salaam.Warioba alisema mtazamo wake ni vyema kuwa na ukomo wa mtu kuwa mbunge, ambapo alipendekeza vipindi vitatu vya miaka mitano mitano yaani miaka 15
No comments:
Post a Comment