Kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambogo wilayani Rorya mkoani
Mara, ambaye anadaiwa kupotea nyumbani kwa imani za kishirikina hatimaye
amepatikana huku akiwa katika hali ya kutisha bila kujitambua na mwili
wake ukiwa umejaa tope jingi, tukio ambalo limevuta mamia ya wananchi wa
kijiji hicho.
Kijana huyo Kenedy oguko mwenye umri wa miaka 22 amekutwa nje ya
nyumba yao asubuhi ya Juni 5 mwaka huu akiwa uchi wa mnyama,ambapo
baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa tangu
kutoweka kwa
kijana huyo siku nne zilizopita,wamekuwa wakimtafuta bila mafanikio huku
wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya Bw Samwel
Kiboye,ambaye ni miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo amewaomba wananchi
kuacha kulipiza visasi kwa kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa ushirikina
bali watumie vyombo vya dola huku mwenyekiti wa kijiji hicho akilaani
vikali vitendo hivyo vya ushirikina vinavyoendelea kijijini hapo hatua
ambayo amesema imesabisha wananchi sasa kuishi kwa hofu kubwa.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza wazee wa jadi kijijini hapo waliagiza kila mwananchi kupita mbele ya kijana huyo na kumpa mkono kama njia moja wapo ya kuwezesha kupata fahamu kitendo ambacho hata hivyo hakikuzaa matunda.
No comments:
Post a Comment