Watoto mapacha wenye umri wa miaka sita, wamekufa baada ya
kutumbukia kwenye kisima cha maji wakati wakicheza.Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema watoto hao walitumbukia kwenye
kisima kilicho jirani na nyumbani kwao.
“Pacha wa kwanza alipoona mwenzake amezama, alikwenda na kutaka kumwokoa mwenzake ndipo naye alipozama,” alisema Kamanda Matei na kuongeza kwamba miili yao ilikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.
No comments:
Post a Comment