Glazer mkubwa amekuwa mgonjwa kwa muda sasa na kuwaachia shughuli za uendeshaji wa United watoto wake wa kiume, Joel na Avram.
Familia
ya Glazer bado wanamiliki Tampa Bay Buccaneers, timu ya mpira wa miguu
ya Marekani waliyoinunua mwaka 1995. Na kwenye tovuti ya Bucs, ambako
zimetangazwa habari za kifo cha Glazer.
Wakati wa umiliki wa Glazer, United imeweza kushinda mataji matano ya Ligi Kuu ya England na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Glazer ameacha mke, Linda waliyefunga naye ndoa mwaka 1961 na watoto na watoto sita, Avram, Kevin, Bryan, Joel, Darcie na Edward.
No comments:
Post a Comment