MKALI wa vichekesho Bongo, Haji Salum ‘Mboto’
ameibuka na kusema kuwa endapo atafariki dunia mwili wake ukaagiwe
katika Viwanja vya TCC Chang’ombe na siyo Leaders kama ambavyo imekuwa
ikifanyika kwa wasanii wengi wanapokufa.
Akizungumza na paparazi wetu kwenye Viwanja vya Leaders
wakati wa msiba wa msanii mwenzake, achel Haule ‘Recho’, Mboto alisema
tayari ameshaacha wosia kwa marafiki zake kwamba siku akifariki dunia
mwili wake uagiwe TCC kwani yeye nyumbani kwao ni Temeke na ndugu zake
wengi wapo huko na endapo wosia huo utakiukwa jeneza lake litagoma
kubebeka.
“Mimi nimeshawaambia marafiki zangu kwamba siku nikifa
mwili wangu uagiwe TCC Chang’ombe kwa sababu ndiyo nyumbani kwetu,
naomba wale niliowaambia walizingatie hilo wakiona linakiukwa wagome na
jeneza langu ligome kubebeka,” alisema Mboto
No comments:
Post a Comment