Mlipuko mkubwa umetokea kwenye meli kubwa ya mafuta nchini Japan
katika Pwani ya Kusini Magharibi mwa bandari ya Himeji na kusababisha
mtu mmoja kati ya wanane waliokuwa ndani ya meli hiyo kupotea huku
wengine wanne wakijeruhiwa vibaya.
Moto mkubwa ulilipuka katikati ya bahari ambapo meli hiyo yenye uzito
wa tani 998 iliyokuwa ikitokea mji wa Hiroshima kuachwa ikielea ndani
ya maji baada ya ajali hiyo na baadae kufatwa na meli za kupambana na
majanga ya moto.
Watu
saba wameokolewa katika ajali hiyo mbaya, wanne wakiuguza majeraha ya
moto kwa mujibu wa shirika la habari la NHK, ambapo kapteni wa meli hiyo
amesema uchunguzi kumtafuta mtu mmoja aliyepotea bado unaendelea.
Afisa
usalama katika Pwani hiyo Koji Takarada amesema chanzo cha mlipuko huo
bado hakijajulikana ambapo shirika la habari NHK limeripoti kuwa
wafanyakazi wa meli hiyo walikuwa wakifanya kazi chini ya meli wakati
mlipuko unatoke
No comments:
Post a Comment