Mjumuiko wa visiwa 1864 vilivyoko kwenye mpaka wa Canada na
Marekani katika mto wa St Lawrence unachora picha nzuri sana ya
kimaumbile na kuonesha utukufu wa Allah aliyewaumbia wanadamu dunia
yenye sura za kuvutia inayoweza kukalika na kuwamiminia humo neema Zake
nyingi sana viumbe Wake mbalimbaliUkubwa wa eneo la visiwa hivyo 1864 unakadiriwa kuwa ni Zaidi ya meli
mraba 40 na wenyeji wake wakuu ni ndege wa majini wanaohama-hama.
Kisiwa kikubwa zaidi kati ya visiwa hivyo kinajulikana kwa jina la Wolfe chenye urefu wa kilomita 29 na upana wa kilomita 9.
Mwaka 2002 eneo linalojumuisha visiwa hivyo lilitangazwa na UNESCO kuwa ni hifadhi ya kimataifa.
Aghlabu ya visiwa hivyo havikaliwi na watu na mara nyingi utapata nyumba moja katika kila kisiwa na wakazi wake wanatumia boti kwenda na kurudi bara.
Nyumba za visiwa hivyo zinatumia umeme wa maji na huduma za simu zinatumia nyaya zilizowekwa chini ya maji kutoka kisiwa kimoja hadi kingine.
Ametukuka Allah, Mbora wa kuumba.
Hapa chini tumeorodhesha baadhi ya picha za visiwa hivyo.

No comments:
Post a Comment