Simplfy language

thanx

Friday, April 4, 2014

LEO KATIKA HISTORIA.

 http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/7bd7ab5dc94fb49a15cbb422ef328afa_XL.jpg
Leo ni Jumamosi tarehe 5 Mfunguo Tisa Jamadul Thani 1435 Hijria mwafaka na tarehe 5 Aprili mwaka 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 58 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 5 Aprili 1956, yalimalizika mashambulizi ya kinyama ya majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina katika eneo la Ukanda wa Gaza. Majeshi ya utawala ghasibu wa Israel, siku ya tarehe 4 Aprili, yalianza kufanya mashambulio makubwa na kuwauwa watu 56 na kuwajeruhi wengine 30 wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee katika kipindi cha siku mbili. Nchi za Magharibi na jamii ya kimataifa hazikutoa radiamali yoyote kuhusiana na jinai hizo za Wazayuni. ***
Miaka 429 iliyopita katika siku kama ya leo, yalifanyika mauaji ya halaiki katika mji wa Haarlem nchini Uholanzi, ambako kilikuwa kitovu cha wapigania uhuru nchini humo. Mauaji hayo yalifanyika kwa amri ya Mfalme wa Uhispania wakati huo aliyejulikana kwa jina la Philip II. Jumla ya watu elfu sita wanaaminika kuwa waliuawa kwenye shambulio hilo. Hatimaye Uholanzi ilijipatia uhuru wake kutoka kwa mkoloni Uhispania 1609.  ***
Katika siku kama ya leo miaka 220 iliyopita, aliuawa Georges Jacques Danton mmoja kati ya vinara wa mapinduzi ya Ufaransa. Danton licha ya kusomea fani ya sheria, alikuwa mhamasishaji mzuri katika kipindi cha mapinduzi ya Ufaransa. Danton alikuwa akiamini kuwa, sanjari na kuzuia machafuko na maafa ya kibinadamu, utawala wa kifalme nchini Ufaransa ulipaswa kutokomezwa. Hatimaye Danton alitiwa mbaroni kwa njama za Maximilien de Robespierre mmoja kati ya vinara wakubwa wa mapinduzi ya Ufaransa ambaye pia alikuwa mshindani wake na kisha akanyongwa. ***
Na miaka 426 iliyopita katika siku kama ya leo Thomas Hobbes mwanafalsafa mashuhuri wa Kiingereza alizaliwa. Alimaliza masomo yake katika Chuo Kikuu Oxford nchini Uingereza na alifanya utafiti mkubwa kuhusiana na fasihi. Hobbes alikuwa mtu mwenye kujiona na aliyependa jaha na madaraka.  Kitabu muhimu cha Thomas Hobbes ni Leviathan. Mwanafalsafa huyo wa Kiingereza alifariki dunia mwaka 1679.

No comments:

Post a Comment