Simplfy language

thanx

Monday, March 31, 2014

LEO KATIKA HISTORIA.....


Leo ni Jumatatu tarehe 29 Jamadil Awwal mwaka 1435 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 31 Machi 2014 Miladia.
www.newinfotz.blogspot.comSiku kama ya leo miaka 66 iliyopita, garimoshi lililokuwa likitoka Cairo Misri likielekea katika bandari ya Haifa huko Palestina lililipuliwa kwa bomu, ikiwa ni katika kuongezeka mauaji ya umati dhidi ya Wapalestina yaliyokuwa yakifanywa na Wazayuni maghasibu. Wapalestina 40 waliuawa na wengine 60 kujeruhiwa katika jinai hiyo iliyofanywa na kundi moja la Kizayuni. Siku nne kabla ya mlipuko huo, garimoshi jingine lililipuliwa huko Palestina na Wazayuni wenye silaha, na kuuwa Wapalestina 24 na kujeruhiwa wengine 61.
Miaka 418 iliyopita kama leo yaani tarehe 31 Machi mwaka 1596, alizaliwa Rene Descartes mwanafalsafa, mwanahisabati na mwanafizikia wa Kifaransa. Descartes alifikia daraja ya uhadhiri wa chuo kikuu baada ya kuhitimu masomo ya falsafa na hisabati. Aidha msomi huyo wa Kifaransa alifanya safari kwa kipindi fulani katika nchi mbalimbali na baadaye aliishi Uholanzi na kuanza kufanya utafiti. Rene Descartes aliitambua hisabati kuwa elimu kamili miongoni mwa elimu nyinginezo na kutaka kutumiwa elimu hiyo katika fani nyinginezo za kielimu. Miongoni mwa vitabu vya mwanafalsafa huyo ni Principles Of Philosophy, The Passions of the Soul na Discourse on the Method.
Na siku kama ya leo miaka 34 iliyopita, nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zilisimamisha uanachama wa Misri katika jumuiya hiyo na nchi nyingi wanachama zikakata uhusiano wao na Cairo. Nchi za Kiarabu zilionesha radiamali hiyo kali kwa Misri baada ya rais wa zamani wa Misri Anwar Sadat kusaini hati ya mapatano ya Camp David na utawala wa Kizayuni wa Israel mwezi Januari mwaka 1978.
 
 


No comments:

Post a Comment