Pages
Simplfy language
thanx
Monday, March 31, 2014
NDEGE ILIYOPOTEA YA MALAYSIA......................
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott amesema kuwa ushahidi uliopo unaashiria kuwa ndege ya Malaysia iliyotoweka ilipotea katika bahari ya Hindi. Abbott amesema ushahidi uliopo unadokeza kuwa ndege hiyo ya Malaysia ilipotelea mahali fulani huko kusini mwa bahari ya Hindi. Waziri Mkuu wa Australia pia ameeleza kuwa zoezi la kuitafuta ndege hiyo ni gumu na kwamba wanaitafuta katika eneo kubwa la bahari kwa kutegemea taarifa chache. Amesema kifaa cha kisasa kabisa cha kiteknolojia kinatumika katika kuitafuta ndege hiyo. Ndege kumi kutoka Australia, China, Japan, New Zeland, Malaysia na Korea ya Kusini zilishiriki katika oparesheni hiyo hapo jana.
Labels:photos
HABARI(News)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment