Pages
Simplfy language
thanx
Monday, March 31, 2014
Mlipuko mwingine.....
Mtu mmoja ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa guruneti huko Nairobi mji mkuu wa Kenya. Barasa Wabomba Mkuu wa Polisi katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi amesema kuwa, mtu huyo aliuawa wakati akitengeneza bomu hilo katika nyumba moja ilioko katika eneo la Pangani mjini humo. Wabomba ameongeza kuwa, jeshi la polisi linawatafuta washukiwa watatu wa mlipuko huo ambao walionekana wakikimbia kutoka kwenye jengo hilo baada ya mlipuko huo. Mkuu huyo wa polisi amesema kuwa, kuna uwezekano mkubwa mtu huyo aliyeuawa ni mwanachama wa kundi la al Shabab, na kusisitiza kwamba kuna uwezekano pia kwa watu watatu waliotoroka kwenye tukio hilo wanafungamana na makundi yenye misimamo mikali nchini Somalia. Barasa Wabomba ameongeza kuwa uchunguzi kuhusiana na tukio hilo umeshaanza, ili kubaini utambulisho wa mtu aliyeuawa na wale waliotoroka. Inafaa kuashiria hapa kuwa, milipuko mingi ambayo imekuwa ikitokea nchini Kenya imekuwa ikifungamanishwa na kundi la al Shabab la nchini Somalia.
Labels:photos
HABARI(News)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment