ZAIDI ya kaya 45 zimekosa makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa mapaa na upepo mkali ulioambatana na mvua ya mawe, hali iliyosababisha wakose mahali pa kuishi. Majanga hayo yalitokea mwishoni mwa wiki iliyopita saa 12 jioni wakati Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Omar Kwaang, Ofisa Mtendani wa Kata ya Mnenia, Abdallah Kavindi, waliposema mvua hiyo imesababisha kaya 45 kukosa makazi. Kavindi alisema mbali ya kuezuliwa nyumba hizo na msikiti, mifugo imekufa na mimea pia imeharibiwa. Alisema mvua hiyo ilikuwa ya maajabu, kwani ilitumia kama dakika tano, ikiwa yenye mabonge ya barafu na kusababisha mimea kuharibika. Kwa upande wake Kwaang aliyekuwa eneo la tukio, alisema serikali inafanya mpango wa kuwasaidia waathirika wa maafa hayo. Alimwagiza ofisa tarafa kufanya tathmini sahihi kwa ajili ya kuwapatia misaada waathirika wote. Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Moza Abeid, alilazimika kutoa msaada wa maturubai kwa ajili waathirika hao.
No comments:
Post a Comment