Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Wednesday, January 15, 2014
Misri: Kura ya katiba yaendelea..............
Misri: Kura ya katiba yaendelea
Raia mmoja wa Misri akionyesha picha ya kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdel Fattah al-Sisi
Raia wa Misri wameendelea na upigaji kura ya maamuzi kwa siku ya pili ikiwa ni
harakati za kupata katiba mpya tangu jeshi la nchi hiyo kuuangusha utawala wa Rais wa zamani Mohammed Morsi.
Jeshi la Misri linashinikiza kura ya ndiyo ili kuhalalisha kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa rais wa Misri Mohamed Morsi, aliyeondolewa madarakani mwezi Julai mwaka 2013.
Vituo vya upigaji kura vimekuwa vikifunguliwa saa tatu asubuhi huku vikosi vya ulinzi vikiimarishwa tangu siku ya Jumanne huku watu tisa wakiripotiwa kuuawa katika vurugu zilizotokea ambapo wengi wa waliouawa ni wafuasi wa Morsi.
Katiba mpya inayotarajiwa kupatikana nchini humo itachukua nafasi ya katiba ya zamani iliyopitishwa na Rais Morsi chini ya chama chake cha Muslim Brotherhood ambacho hivi karibuni kimetajwa kuwa ni kundi la kigaidi.
Wanajeshi wapatao 160,000 na polisi 200,000 wamesambazwa maeneo mbalimbali nchini humo kwa lengo la kudhibiti usalama
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment