Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Wednesday, January 15, 2014
PIKIPIKI YAUA NA KUJERUHI JIJINI DAR.........
MTU mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya kugongwa na pikipiki jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 1 asubuhi katika maeneo ya Moshi Bar baada ya pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye hakutambulika jina kuwagonga watu hao.
Minangi alisema dereva huyo alikuwa anatokea Kwa Mahita akielekea Kwa Masaka, alipofika maeneo hayo aliwagonga watembea kwa miguu hao ambao ni Victor Anthony mwenye umri wa mwaka 1 na Mwanahawa Abdallah (43) waliokuwa wamekaa nje ya kibanda pembezoni mwa barabara.
Minangi alisema ajali hiyo iliwasababishia majeraha mbalimbali, na Anthony alifariki dunia wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya Amana.
Alisema Mwanahawa alibainika kuvunjika mkono wa kulia na anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment