Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Tuesday, January 14, 2014
TAZAMA ALICHOKIZUNGUMZA WENGER KUHUSU MATOKEO.......
Wenger atetea matokeo ya vijana wake
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger, amesema mpangilio wa mechi ulisababisha klabu hiyo kucheza mechi nne bila ushindi wowote.
Lakini klabu hiyo ilimaliza ukame huo kwa kushinda mechi ya ya Alhamisi dhidi ya West Ham.
Kocha huyo amesema klabu yake imecheza mechi sita katika kipindi cha siku ishirini na tatu.
''Imekuwa wakati mgumu kwetu, lakini kilichosababisha sisi kutoandikisha matokeo bora ni wingi wa mechi'' Alisema Wenger.
Arsenal ilianza kampeini yake mwezi huu kwa kuishinda Hull City kwa magoli mawili kwa bila, lakini juhudu zao za kujinyakuliwa kombe lao la kwanza kwa zaidi ya miaka tisa, zilianza kutumbukia nyongo pale ilipozoa alama mbili baada ya kucheza mechi tatu.
Mikel Arteta
Ililazwa 6-3 na Manchester City kabla ya kutoka sare na Everton na Chelsea.
Arsenal pia ililazwa magoli mawili kwa yai na Napoli kwenye mchuano wao wa mwisho wa makundi ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya, hata hivyo vijana hao wa Wenger walifuzu kwa raundi ya muondoano licha ya matokeo hayo.
Mapema mwezi huu mcheza kiungo wa Arsenal Mikel Arteta alihoji uamuzi wa wasimamizi wa ligi hiyo wa kuweka mechi yao na Manchester City kuchezwa wakati wa chakula cha mchana, akidai kuwa wachezaji walikuwa na muda mfupi sana kujitayarisha baada ya mechi yao na Napoli siku mbili zilizotangulia
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment