Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Tuesday, January 14, 2014
Mlipuko wawaua 17 ..............
Mlipuko wawaua 17 ..............
Boko Haram limekiri kufanya shambulizi hilo
Watu kumi na saba wamefariki mwenye mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari mjini Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram, limekiri kufanya shambulizi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa za jeshi mshukiwa mmoja amekamatwa.
Mlipuko huo ulitokea karibu na soko moja mjini
humo. Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa waliwaona watu wakitoroka kutoka eneo hilo nguo zao zikiwa na damu.
Kundi la Boko Haram, limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara Kaskazini mwa Nigeria likiishinikiza serikali kukubali sheria za kiisilamu kutumika katika eneo hilo ambako wakazi wake wengi ni waumini wa kiisilamu.
Miili ilionekana ikiwa imetapakaa kote huku shahidi mmoja akiambia BBC kuwa alisikia mlipuko mkubwa uliofatiwa na milipuko mingine midogomidogo
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment