Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Tuesday, September 10, 2013
Wazazi wamuua mtoto
Wazazi wamuua mtoto waliyemuasili
Carri Williams amepatikana na makosa mabaya zaidi
Wazazi wawili wamehukumiwa kwa kosa la mauaji ya msichana waliokuwa wamemuasili kutoka nchini Ethiopia.
Larry na Carri Williams kutoka jimbo la Washington, walimnyima chakula na kumchapa msichana Hana Williams hadi alipofariki katika bustani ya nyumba yao mwezi Mei mwaka 2011.
Mawakili wa utetezi walikubali kuwa wazazi hao walikuwa wazazi wabaya, lakini akaitaka mahakama kujua kuwa wawili hao sio wahalifu.Pia walishtakiwa kwa kosa la mauaji ya mvulana mdogo aliyekuwa mdogo wa msichana huyo ambaye pia walikuwa wamemuasili kutoka nchini Ethiopia.
Kulingana na stakabadhi kumhusu Hana, msichana huyo angekuwa na umri wa miaka 13 wakati wa kifo chake.
Wazazi hao walilaumiana wakati wa kesi hiyo kulingana na Skagit Valley Herald.
Alipatikana na hatia ya mauaji ingawa jopo la majaji halingeweza kutoa uamuzi kuhusu hukumu watakayopata wawili hao.
Wawili hao walioishi mjini Sedro-Woolley, huenda wakafungwa maisha jela.
Taarifa zinazohusiana
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment