Simplfy language

thanx

Saturday, September 13, 2014

INASIKITISHA MAUAJI YA KUTISHA KWA IDADI KUBWA..

Watu zaidi ya elfu tano wameuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) tangu mwezi Disemba mwaka jana, wakati nchi hiyo ilipotumbukia katika hali ya machafuko.

Hayo ni kwa mujibu wa takwimu mpya. Associated Press imegundua kuwa, mapigano kati ya makundi hasimu ya kikabila katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 5,186 katika muda wa miezi tisa iliyopita.
Takwimu za Associated Press zimepatikana kwa kutegemea watu walioshuhudia machafuko katika jamii zaidi ya 50 zilizoathiriwa zaidi na machafuko huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na vilevile kwa kuhesabu viwiliwili vya wahanga.

Cha kushangaza ni kuwa watu hao wote waliuliwa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati licha ya kuwepo vikosi vya kimataifa vya kulinda amani nchini humo.

No comments:

Post a Comment