Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Monday, July 7, 2014
HALI YACHACHAMAA NIGERIA::Jeshi la Nigeria lamuua kiongozi wa Boko Haram.....
Mmoja wa viongozi wa kundi la Boko Haram ameuawa katika mapigano ya jana usiku katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria.
Wakizungumza na vyombo vya habari, wakazi wa jimbo la Kaduna wameeleza kuwa vikosi vya usalamam vya Nigeria viliivamia nyumba ya kiongozi huyo wa Boko haram aliyefahamika kwa jina la Othman Sariki ili kumtia mbaroni, hata hivyo kamanda huyo wa Boko Haram alipambana kwa silaha na vikosi hivyo vya usalama na hatimaye akauawa pamoja na kaka yake. Jeshi la Nigeria juzi lilitangaza kuwa limewauwa wanamgambo wa Boko Haram zaidi ya 50 katika mapigano kati ya pande mbili hizo. Wanajeshi na raia kadhaa waliuawa pia kwenye mapigano hayo yaliyojiri katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment