Jaji Warioba ambaye aliwahi kuongoza Tume ya Rushwa iliyoundwa na
Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, alisema amani ya Tanzania
ikivurugika kutokana na makundi kupingana katika mchakato wa Katiba
wanasiasa ndio watakaonyooshewa vidole.
- Kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?
- Wapeni majibu wananchi kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano?
- Elezeni kwa nini Katiba imevunjwa, madaraka ya Rais kuchukuliwa na marais wawili katika nchi moja?
- Tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi na kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?
- Kwa nini wanawatuhumu uongo yeye na Joseph Butiku kuwa walikuwa wajumbe wa Tume za Kisanga na Nyalali zilizopendekeza serikali tatu?
- Kwa nini hawataki kuzungumzia yaliyomo katika rasimu bali wanadai imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba?
- Waeleze kwa nini wanadai Tume imeingiza maoni yake, wakati iliyakusanya kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?
No comments:
Post a Comment