KOMEDIAN mahiri Bongo, Haji Salum ‘Mboto’ amefunguka
kuwa Saguda alikijua kifo cha mpenzi wake, Sheila Haule ‘Recho’
kutokana na kauli zake alizokuwa akimwambia pindi alipokuwa akimuomba
acheze filamu na mkewe kisha akafariki kabla haijatoka.
Akizungumza katika mahojiano maalum aliyofanya na paparazi wa Global TV Online (inapatikana kupitia
, Mboto alisema kuwa wakati Recho anakaribia kujifungua, Saguda
alimfuata na kumuomba amsaidie kucheza naye filamu lakini akakataa.
“Saguda alinibembeleza sana mwisho wa siku akaniambia Mboto huwezi
jua nini Mungu amekipanga mbele, kubali kucheza na mke wangu, kiukweli
nilikubali kwa shingo upande na nikawa nacheza nje ya mudi kutokana na
kwamba sikuipenda ile hali ya Recho kwa kuwa niliogopa tunaweza
kubishana au kugombana na yeye ni mjamzito, maskini kumbe ndiyo ilikuwa
filamu yake ya mwisho,” alisema Mboto huku akibubujikwa na machozi.
Kwa mujibu wa Mboto, hiyo ilikuwa ni filamu ya tatu kushiriki na wahusika wakuu kufariki dunia. Ya kwanza ni Kijiji cha Tambua Haki (Steven Kanumba), The Boss (Adam Kuambiana) na hiyo ya mwisho itakayojulikana kwa jina la Fedheha
No comments:
Post a Comment