Simplfy language

thanx

Monday, June 2, 2014

KAULI NZITO ILIYOWASHITUA WENGI..

Mjinii Iringa kwenye viwanja vya Mwembetogwa, Mh Mwigulu Nchemba alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, alisema kuwa Watanzania wana uhuru mkubwa sana wa kuongea mpaka wanakosa adabu hata kwa wazee wao “..najua mnaona natumia lugha kali, lakini ndio kawaida yangu kusema ukweli, …natamani niwe Rais wa nchi hii ili niwafundishe adabu Watanzania, ndio!” Labda inawezekana alimaanisha kuwafundisha adabu Watanzania fulani, lakini kwakuwa alikuwa akiongea kwa jazba aliteleza ulimi, au alimaanisha hivyo. Watu waliohudhuria mkutano huo walipigwa na butwaa, aliliona hilo na kubadilisha mada haraka. Aliwafurahisha watu pale aliposema”..kule kwetu Singida, ng’ombe mpole ndie anaekamuliwa sana maziwa, lakini yule mkorofi anaachwa, kadhalika (serikali) inawatoza kodi wajasiriamali wadogo bila msamaha lakini wawekezaji wakubwa wanasamehewa mabilioni ya fedha!) suala hilo ameahidi kupambana nalo.

No comments:

Post a Comment