Simplfy language

thanx

Tuesday, June 17, 2014

AGIZO ZITO KUTOKA KWA RAIS KIKWETE..



Rais  Kikwete ambaye amesema kitendo hicho ni cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani, amekitaja kuwa ni cha woga kisicho na ustaarabu, kisichokubalika katika dunia ya sasa.

Alisema hayo katika salamu za rambirambi alizotuma jana kwa Rais Ali Mohamed Shein wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Bomu hilo lilirushwa katika shughuli ya kidini iliyokuwa ikifanyika katika eneo la Darajani , mjini Unguja. Miongoni mwa majeruhi, yumo mhubiri wa amani ajulikanaye kama Sheikh Ahmed Haidari Jabir wa Zanzibar.
“Hicho ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani, ni kitendo cha woga na kisicho na ustaarabu na wala hakikubaliki katika dunia ya sasa,” alisema Rais Kikwete  na  kuongeza:
“Hiki ni kitendo kilichofanywa na watu waoga, wasio na ustaarabu wa aina yeyote ile.”
Alikemea wanaofanya vitendo hivyo na akahimiza watu kuwa wastaarabu, wavumilivu na kuheshimu imani na mitizamo ya watu wengine hata kama hawakubaliani nao.
Akiendelea kulaani, alisema amesikitishwa zaidi na watu hao wasio na ustaarabu ambao wamefanya kitendo hicho cha kihalifu kwenye shughuli ya kidini ambapo ndipo mahali panapostahili amani, uvumilivu na unyenyekevu zaidi kwa kuwa ni wakati ambapo binadamu anapofanya mawasiliano na muumba wake.
Alihimiza polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki wahusika wa tukio hilo. Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai wa Zanzibar, Yussfu Ilembo, aliyekufa papo hapo ni Muhammad Mkombalaguha (26), mkazi wa Tanga.
Kutokana na tukio hilo, polisi visiwani humo ilitangazia hali ya hatari kwa  watu waliohusika na shambulio hilo. Ilielezwa kwamba uchunguzi umeanzia kwenye mabaki ya vitu vilivyokutwa katika eneo la tukio.
Miongoni mwa vielelezo vilivyokusanywa ni pamoja na vipande vya mabaki ya gundi ya karatasi na vitu vingine ambavyo vinasadikikwa vimetumika kutengeneza bomu hilo.
Mtu aliyekufa pamoja na majeruhi, walikutwa na mkasa huo wakati wakitoa Msikiti wa Darajani baada ya Ibada ya Swala ya Isha inayoswaliwa kuanzia saa 1:45 usiku na kuendelea.
Baada ya kumalizika ibada hiyo, walitoka msikitini na kufika eneo la Darajani wakisubiri gari na ndipo mlipuko mkubwa uliposikika ambao unasadikiwa kuwa ni bomu.
Katika hatua nyingine, akiwa mkoani Dodoma juzi, Rais Kikwete aliwataka Watanzania kuendelea kulinda na kupigania amani iliyopo kwa ustawi na usalama wa nchi .
Rais Kikwete alisema hayo juzi kwenye uzinduzi wa tamasha la uzalendo lililoasisiwa na wasanii wa muziki na filamu nchini ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa video ya wimbo maalumu wa Muungano wa Tanzania na Zanzibar.
Alisema uzalendo kwa Watanzania ndiyo njia pekee ya kufanya taifa liendelee kutunukiwa hadhi ya kisiwa cha amani duniani.
Katika tamasha hilo lililofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Rais Kikwete alisema ili kuwaenzi waasisi wa taifa, ni lazima kudumisha misingi ya amani na kujitolea kizalendo kulilinda na kulitetea taifa kama walivyofanya waasisi Mwalimu Julius Nyerere na Shehe Abeid Amani Karume.

No comments:

Post a Comment