 MAHABUSU wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, 
wameleta kizaazaa baada ya kujaribu kutoroka na kukimbilia kwenye 
mlingoti wa Bendera ya Taifa nakuing’ang’ania kisha kuvua nguo na mmoja 
wao kubaki mtupu.
MAHABUSU wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, 
wameleta kizaazaa baada ya kujaribu kutoroka na kukimbilia kwenye 
mlingoti wa Bendera ya Taifa nakuing’ang’ania kisha kuvua nguo na mmoja 
wao kubaki mtupu.
Tukio hilo limetokea leo majira
 ya saa 4:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya 
Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati mahabusu hao walipofikishwa 
kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao, lakini ghafla walipofika kwenye 
viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbiyo kuelekea kwenye mlingoti wa 
Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo.
Inspector
 Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, 
kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha 
mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi.

Inspector
 Henry (shati la bahari) akiwa na Inspector Veda (mwenye koti) 
wakisikiliza hoja za Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na
 kubaki mtupu akiwa ameng’ang’ania mlingoti wa Bendera ya Taifa

Ushawishi ukiendelea.

Mahabusu
 Thobiasi Warioba (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu 
katu waking’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza 
kuzungumza na waandishi wa Habari.

Wananchi wakiwa wamefurika viwanja vya mahakama.

Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama.

Nje ya Mahakama kuelekea lango kuu.

Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama.
 


 
 
No comments:
Post a Comment