Simplfy language

thanx

Friday, May 23, 2014

MNYIKA BUNGENI.....

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, ameitaka serikali kutoa maelezo ya  matumizi ya mkopo wa Sh. bilioni 40 sawa na Dola milioni 27 iliyotolewa kwa ajili ya kununua mitambo mipya ya kiwanda cha nguo cha
Urafiki pamoja na  kujibu tuhuma ya kununua mitambo chakavu badala ya mitambo mipya.
Pia, Mnyika aliitaka  ieleze mchakato wa kutafuta mwekezaji mpya ulivyofanyika unaohusu kampuni ya China inayomiliki hisa asilimia 51 katika kiwanda hicho ambao uligubikwa na usiri na utata mkubwa.

Taarifa hiyo ambayo aliiwasilisha katika ofisi ya Spika wa bunge Mei 16, mwaka huu pia anamtaka Meneja Mkuu Msaidizi Nassoro Baraza, na Meneja wa Utawala Moses Swai wa kiwanda hicho,  wawajibike kwa umma kueleza namna walivyoshiriki katika kuwezesha matumizi mabaya ya mali za kiwanda.

Kadhalika, aliwataka waweke hadharani mikataba yote tata ya upangishaji wa maeneo pamoja na uuzaji kiholela wa mali za kampuni.

Mnyika alisema tangu kiwanda hicho kipate mbia mpya kimekuwa  na matatizo makubwa na kwamba kwa ajili ya kukinusuru, Serikali iliingia makubaliano na Serikali ya China kutoa mkopo wa Dola milioni 27 (Sh. bilioni 43).
Aliongeza kuwa Kiwanda hicho pia kinaendelea kukatwa vipande na kuwa na viwanda vidogo vidogo vingi vinavyodaiwa kumilikiwa na raia wa China, ambao wanatengeneza vitu vidogo vidogo kama viroba na viatu aina ya yebo yebo.  Kadhalika, alisema hata maeneo mengi yamekodishwa kwa Wachina na  Watanzania kinyume cha lengo la awali la wakati kinajengwa miaka ya sitini kutengeneza nguo.

No comments:

Post a Comment