Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Tuesday, May 27, 2014
INASIKITISHA ...SOMA KAULI ZA WASANII KUHUSU KIFO CHA MSANII RECHO..
Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule ‘Recho’ (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam.
Habari zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo.
Hizi ni kauli za baadhi ya mastaa
Shilole
Staki kumkufur mwenyez Mungu wangu! Ila kazi yake haina makosa tulimpenda ila mwenyezi Mungu kampenda zaid! Dah inauma sana pole Saguda kwa mtihan uliokupata!Ila tupo pamoja kwa kipind hik kigumu 1h
Zamaradi Mketema
OMG!!! Sijawahi kushtuka kama hivi… nasikitika kutangaza MSIBA mwingine mkubwa ndani ya BONGO MOVIE!!! RACHEL HAULE hatunae tena duniani… AMEFARIKI Asubuhi ya leo… INALILLAHI WAINAILAIHI RAJIUN…. pumzika kwa Amani mama… MUNGU YUPO jamani!!!!! 2h
Jacky Wolper
Recho haule me nakutambua kma sheilah kipnd ni rafk yangu kipenz nilikua napenda kukuita sheila .R.i.p sheilah umeamua kumzalia mwanaume unaempenda saguda lkn aikufanikiwa mtoto akaiga dunia na sasa umefwata wewe jaman ni pigo kubwa kwakijana yule na kwa famly na sisi bongo movie pia..Mungu amekupenda zaidi ..pole saguda shemeji yetu…R.I.P sheilah 8min
Riyamaally
Innalilahi wainna ilaihirajiun mbele yako nyuma yetu kazi ya mungu hainamakosa kila nafsi itaonja umauti mungu akuweke unapo stahili maa amen daima tutakukumbuka na pengo lako halitafutika kamwe pumzika kwa amani pole sana kaka saguda mungu akujalie sunira na uvumilivu amin pole familia pole bongo muvi na tuwe pole kwa sote kila alie guswa na msiba huu jamaa na marafiki ,,,,natue pole kwa sote kazi yake mola daima haina makosa mungu ameleta nae amechukua jina lake lihimiliwe milele amin 5min
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment