Pages
Simplfy language
thanx
Saturday, April 5, 2014
ZAIDI YA WATOTO 1520 WAMEUWAWA....
Askari wa utawala haramu wa Israel wameuawa zaidi ya watoto 1,520 wa Palestina na kuwajeruhi wengine karibu 6,000 tokea mwaka 2000
.
Hayo yamedokezwa na Waziri wa Afya wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Kamal al-Sharafi alipokuwa akizungumza Jumamosi kwa mnasaba wa Siku ya Watoto wa Palestina. Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 14 iliyopita, zaidi ya watoto 10,000 Wapalestina wametiwa mbaroni na vikosi vya utawala wa Israel ambapo hivi sasa kuna watoto 200 wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za utawala huo ghasibu.
Waziri huyo wa Palestina ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kuwalinda na kuwatetea watoto hao Wapalestina. Mwaka jana Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Watoto UNICEF ilielezea wasi wasi wake kuhusu ukatili wa utawala haramu wa Israel dhidi ya watoto wa Palestina. UNICEF ilisema vitendo vya Israel dhidi ya watoto wa Palesitna ni vya kinyama na dhidi ya ubinaadamu na kwamba utawala huo unakiuka mikaba ya kimataifa kuhusu haki za watoto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment