Simplfy language

thanx

Tuesday, April 15, 2014

LEO KATIKA HISTORIA....


Leo ni Jumanne tarehe 15 Jamadithani 1435 Hijria sawa na Aprili 15, 2014.
Siku kama ya leo miaka 20 iliyopita, ulitiwa saini mkataba wa kuanzisha Shirika la Biashara Duniani (WTO)
nchini Morocco. Utangulizi wa kuasisiwa shirika hilo ulifanywa na Marekani na Uingereza wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na kwa msingi huo, mwaka 1947 nchi 23 zilizoendelea zilitia saini makubaliano ya kuanzisha GATT. Makubaliano hayo yalisisitiza juu ya kufanyika mazungumzo ya kupunguza ushuru wa forodha, vipingamizi vya biashara na kuondoa vizuizi vya biashara huru. Baadaye jumuiya ya GATT ilibadilishwa jina na kuwa WTO na hati yake ilianza kutekelezwa Januari mwaka 1995. Hata hivyo Marekani na nchi nyingine za Magharibi zimeliteka shirika hilo la kibiashara duniani na zinalitumia kwa faida na maslahi yao wenyewe.
Miaka 28 iliyopita katika siku kama hii ya kama leo, Marekani iliishambulia miji ya Tripoli na Benghazi nchini Libya. Kisingizio kilichotumiwa na Washington kufanya mashambulizi hayo ya anga ni kuwa Libya ilihusika katika mlipuko uliotokea kwenye mkahawa mmoja mjini Berlin, Ujerumani ambapo askari watatu wa Marekani waliuawa. Raia kadhaa ambao hawakuwa na hatia yoyote waliuawa katika mashambulizi hayo ya Marekani katika miji ya Tripoli na Benghazi. Mashambulizi hayo yaliamsha hasira za Waislamu na kulaaniwa vikali na jamii ya kimataifa.
Na Siku kama ya leo miaka 664 iliyopita, sawa na tarehe 15 Jamadu Thani mwaka 771 Hijria, alifariki dunia Fakhrul Muhaqqiqiin, faqihi na msomi mkubwa wa Kiislamu. Mwanachuoni huyo alizaliwa mwaka 682 Hijria na kupata elimu ya kidini kwa mzazi wake Allamah Hilli na wanachuoni wengine wa zama zake. Fakhrul Muhaqqiqiin ameacha vitabu vingi na miongoni mwavyo ni Manbaul Asrar na Tahswilul Najah.

No comments:

Post a Comment