Simplfy language

thanx

Tuesday, April 1, 2014

LEO KATIKA HISTORIA...



Leo ni Jumanne tarehe Mosi Jamadi Thani 1435 Hijria sawa na Aprili Mosi, 2014.
Siku kama ya leo miaka 35 iliyopita, sawa na tarehe 12 Farvardin mwaka 1358 Hijiria Shamsia, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wananchi Waislamu wa Iran walishiriki katika kura muhimu na ya kihistoria ya maoni ya kuamua mfumo uliotakiwa kutawala hapa nchini. Kura hiyo ya maoni ilifanyika kwa muda wa siku mbili. Katika kura hiyo ya maoni asilimia 98.2 ya wananchi Waislamu wa Iran waliunga mkono kuanzishwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu nchini. Kuanzia hapo, kila mwaka ifikapo tarehe 12 mwezi Farvardin, Iran huadhimisha siku hii inayojulikana hapa nchini kwa jina la "Siku ya Jamhuri ya Kiislamu."
Miaka 69 iliyopita mwafaka na siku hii ya leo, vikosi vya jeshi la Marekani vilifanya mashambulizi makubwa katika kisiwa cha Okinawa huko Japan. Mashambulizi hayo yaliyofanywa na wanajeshi wa Marekani mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia yanahesabiwa kuwa vita vikubwa zaidi vya baharini na nchi kavu kuwahi kushuhudiwa kati ya Marekani na Japan. Meli 1300 na karibu ndege za kivita za Marekani elfu 10 zilishiriki kwenye vita hivyo vilivyodumu kwa muda wa siku 83.
Na siku kama ya leo miaka 776 iliyopita alifariki dunia faqihi, mwanahistoria na mwanafasihi wa Kiislamu wa Andalusia Ibn Sayyidunnas. Alizaliwa mwaka 597 Hijria kandokando ya mji wa Seville katika Uhispania ya sasa na kupata elimu katika eneo hilo. Ibn Sayyidunnas alitumia sehemu kubwa ya umri wake katika kufundisha na kulea wanafunzi wengi. Mwanahistoria huyo wa Andalusia alikuwa pia hodari katika kuandika mashairi na katika fasihi na aliandika mashairi mengi kumsifu Mtume Muhammad (saw).
Miongoni mwa vitabu vya msomi huyo ni kile kinachozungumzia sira na maisha ya Nabii Muhammad (saw).


No comments:

Post a Comment