Simplfy language

thanx

Tuesday, April 1, 2014

HALI INATISHA WATU 6 WAMEKUFA.......




Watu sita wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya
milipuko ya mabomu iliyotokea jana katika eneo la Eastleigh mjini Nairobi Kenya. Kamanda wa Polisi Kaunti ya Nairobi Benson Kibue amethibitisha kuuawa watu sita kwenye milipuko hiyo.
Milipuko hiyo imetokea katika hali ambayo, juzi mtu mmoja aliuawa wakati alipokuwa akitengeneza bomu kwenye nyumba moja iliyoko katika mtaa wa Eastleigh jijini Nairobi. Hadi sasa hakuna mtu au kikundi chochote kilichotangaza kuhusika na shambulio hilo la jana, lakini kidole cha tuhuma kinaelekezwa kwa kundi la al Shabab la Somalia ambalo lmekuwa likitekeleza mashambulio nchini Kenya.
Eneo la Eastleigh linakaliwa na raia wengi wa Kenya wenye asili ya Kisomali.
Wakati huohuo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya atafanya safari ya wiki mbili katika nchi kadhaa za Ulaya na Kiafrika, ikiwa ni pamoja na kushiriki kikao cha siku tatu cha wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kinachoanza kesho Jumatano nchini Ubelgiji.
Manoah Esipisu Msemaji wa Rais Kenyatta amesema kuwa, Rais wa Kenya licha ya kushiriki mkutano huo wa Ubelgiji, atazitembelea nchi za Uingereza, Uturuki na Rwanda.
Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika na Ulaya utajadili zaidi masuala ya amani, usalama, uwekezaji, mabadiliko ya hali ya hewa na wahajiri.

No comments:

Post a Comment