Simplfy language

thanx

Wednesday, March 26, 2014

WATANZANIA 15 WAMEHUKUMIWA KIFO.................

www.newinfotz.blogspot.com
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youqing wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo siku ya Jumanne tarehe 25 Machi, 2014. Mkutano huo ulizungumzia maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano wa kidiplomasia  kati ya Tanzania na China na mafanikio ya ziara ya Rais wa China aliyoifanya nchini ambayo imetimiza mwaka mmoja.

Sehemu ya waandishi wa habari walioshiriki mkutano wa waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo. 

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali, Bw. Assah Mwambene wakati wa Mkutano wa Pamoja na waandishi wa habari kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Balozi wa China.

Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bibi Mindi Kasiga akisikiliza kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa. wengine ni maafisa wa Ubalozi China.

Baadhi ya maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje walioshiriki mkutano huo. 

Picha ya pamoja, kutoka kulia ni Balozi wa China, Mhe. Lu Youqing; Katibu Mkuu, Bw. John M. Haule; Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Nathaniel D. Kaaya; Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bibi Mindi Kasiga na Afisa kutoka Ubalozi wa China.
******** 
Matukio ya kukamatwa kwa Watanzania nchini China kwa kesi za biashara ya dawa za kulevya yana idadi kubwa sana ndani ya hii miaka mitano iliyopita. 

Miezi miwili iliyopita Balozi wa Tanzania China alithibitisha kwamba Watanzania wasiozidi 200 ndio wamefungwa kwenye magereza mbalimbali ya China kutokana na kesi tofautitofauti ila dawa za kulevya ndio zinaongoza
 
Balozi huyo alisema kwa wakati huo hakuwa na rekodi yoyote ya Mtanzania kuhukumiwa kunyongwa au yeyote ambae tayari ameshanyongwa na kwamba kwa taarifa zaidi Wizara ya mambo ya nje itafutwe.
 
Baada ya hayo yote, hatimae katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje John Haule March 25 2014 ametaja jumla ya Watanzania waliokamatwa kwa kesi ya dawa za kulevya kwa kusema:

“Tuna Watanzania wengi tu ambao wapo kwenye magereza kule China japo tumeshindwa kwa harakaharaka kupata idadi ya waliojihusha na shughuli ya dawa za kulevya lakini kuna rekodi fupi tulizonazo sasa hivi….
 
“Katika Magereza ya China mpaka February 2014, tumepewa taarifa na Mamlaka za China kwamba wapo Magerezani Watanzania 177 ambapo 15 kati yao wamehukumiwa kunyongwa kutokana na biashara hiyo ya dawa lakini niseme tu wenzetu wa Serikali ya China wanatuthamini sana kama sisi tunavyowathamini’
 
“Wenzetu wa China wanathamini zaidi uhusiano wetu na ndiyo maana hata wale  watanzania wachache waliohukumiwa kunyongwa hawajanyongwa mpaka leo na hatutegemei kama watanyongwa, naamini sanasana watafungwa kifungo cha maisha gerezani”

No comments:

Post a Comment