Simplfy language

thanx

Wednesday, March 26, 2014

Polisi kuwapiga risasi washukiwa...........

Polisi kuwapiga risasi washukiwa wa ugaidi
        
     
               
Polisi imepanua operesheni za kuwasaka wahalifu waliohusika kushambulia kanisa huko
 Likoni mjini Mombasa siku ya Jumapili hadi katika maeneo ya jirani ya Kwale na Kilifi, huku Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa akitoa amri ya kupigwa risasi mtu yeyote anayeshukiwa kuwa gaidi. Marwa amedai kuwa haina manufaa kupelekewa washuhikiwa wote wa ugaidi mahakamani lakini ni vigumu kuwahukumu na kupata ushahidi katika kesi hizo. Akizungumza moja kwa moja katika Kaunti ya Mombasa Kamanda wa Kaunti ya Mombasa, Joseph kitur ameeleza kuwa, Marwa amesema, amri ya kupigwa risasi washikiwa wa ugaidi imechukuliwa kwa kuwa magenge ya watenda jinai yana ushawishi mkubwa kwenye jimbo hilo na kwamba ni haki kuuawa watenda jinai hao ikilinganishwa na unyama wanaowatendea wahanga.
Kwa mujibu wa Marwa, hadi sasa polisi wamewaua wahalifu 7 sugu  waliokuwa kwenye orodha yao ambapo mmoja wao alipigwa risasi Jumapili wakati  kanisa la Likoni liliposhambuliwa.


No comments:

Post a Comment