Simplfy language

thanx

Friday, September 12, 2014

WARIOBA ASHAURI BUNGE LA KATIBA LISITISHWE...

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania, Jaji Joseph Warioba, amesema  kuwa ni vyema Bunge Maalumu la Katiba likasitishwa kwani Katiba bora haiwezi kupatikana kwa muda wa wiki mbili.


Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja siku moja tu baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kumtaka Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kulisitisha, huku mwenyewe akisema litaendelea na hadi kufikia Oktoba 4 Katiba inayopendekezwa itapatikana. Jaji Warioba aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameeleza kushangazwa kwake na haraka waliyonayo wajumbe wa Bunge hilo wakati wanajua kuwa Katiba haiwezi kupatikana kwa muda uliobakia.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema kwamba, hakuna sababu ya kuharakisha mchakato huo na kuwa hata ikibidi baada ya miaka 100, lakini la muhimu ni kupatikana Katiba bora.

No comments:

Post a Comment