Simplfy language

thanx

Wednesday, September 10, 2014

WANAFUNZI HOSTELI CHUO CHA HABARI WATAKI KUTUNZA MAZINGIRA....

 Aliyeva shati jeupe ni Waziri Emmanuel Ndenshau kiongozi wa hosteli za Loliondo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha akihojiwa na mwandishi wa blog hii Gift Adison.picha na TEODORA MASSAWE.


Baadhi ya wanafunzi wa hosteli wakiwa katika eneo la kantini..picha na TEODORA MASSAWE.



Baadhi ya wanafunzi wa hosteli wakiwa wanajisomea katika eneo la hosteli..picha na TEODORA MASSAWE.


Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha wanaoishi hosteli za loliondo wameomba uongozi wa hosteli hiyo kuwapatia vifaa vya kufanya usafi kwa wakati ili kuweka mazingira safi.

Wakizungumza na waandishi wa habari mapema leo wamesema kuwa wamekuwa wakicheleweshewa vifaa vya kufanya usafi kitendo kinachowapelekea mazigira ya hosteli hiyo kotoridhisha.

Mmoja kati ya wanafunzi hao aliyejitambulisha ZIARA NYATU amesema kuwa maisha ya hosteli ni mazuri endapo mazingira yatakuwa safi ili kuwaepusha na magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu
   ``Maisha ya hositeli yananisaidia kuwa huru kitaaluma kwani nakuwa na muda  mwingi wa kubadilishana  mawazo na wezangu na kufanya mazoezi ya vitendo katika kituo cheti cha redio hapa chuoni``Alisema nyatu.
                   
 Pia ameeleza changamoto wanazokabiliana nazo  kuwa ushirikiano hafifu kwa wanafunzi wengine kawa kutoshiriki katika ufanyaji usafi, tabia ya wizi, uhaba wa maji safi ya kunywa, na pia kuwapelekea baadhi ya wanafunzi kuzidi kuhama kutoka katika hosteli

``wanafunzi wengi wanatoka sehemu mbalimbali kila mtu akiwa na tabia yake hivyo inachukua mda kumbadilisha mtu kuendana na mazingira Fulani ambayo hajayazoea kama vile kufannya usafi wa jumla, na kuchoma taka pale zinapoonekana kujaa`` alisema nyatu 
  
Kwa upande wa kiongozi wa hosteli ya loliondo bwana Emmanuel Ndanshau amesema kuwa amekuwa akifanya vikao  chumba hadi chumba ili kuweza kuwashauri na kuwaonya pale wanapokwenda kinyume sheria na utaratibu wa hosteli

Bwana Ndanshau ameeleza matatizo anayokumbana nayo katika mazingira hayo ni gari la taka kuchelewa kufika kwa wakati pamoja na uhaba wa maji safi ya kunywa ingawa maji yanayopatikana ni ya kisima kwani sio bora kwa afya zao

No comments:

Post a Comment