Simplfy language

thanx

Thursday, September 4, 2014

LOH!! WAALIMU TZ WALILIA VYEO MAANDAMANO YA NCHI NZIMA RASMI WAAHIDIWA.......


Baraza la Taifa la Chama cha Walimu  nchini Tanzania (CWT), limetoa siku 14 kwa wakurugenzi wa halmshauri nchini humo kuwapa barua za kuwapandisha vyeo walimu wanaostahili, la sivyo watafanya maandamano nchi nzima.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, amesema kuwa, maazimio ya baraza hilo yalifikiwa tarehe 28 mwezi uliopita mkoani Morogoro. Mukoba, amesema ifikapo Septemba 15 mwaka huu kama wakurugenzi watakuwa hawajawapatia walimu wanaostahili barua za kuwapandisha vyeo, basi watarajie maandamano ya walimu kwenye ofisi zao. “Baraza limetoa siku 14 kuanzia siku ya kikao na ifikapo siku ya tarehe 15 kama walimu wanaostahili kupandishwa vyeo watakuwa hawajapewa barua zao, kutafanyika maandamano ya nchi nzima kuelekea kwa wakurugenzi wa halmashauri kudai barua hizo, hatupendi hali hii itokee lakini hatufurahishwi na hali ya kutojali haki zetu,” amesisitiza Rais wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu nchini Tanzania. Ameongeza kuwa, hata nyongeza ya mishahara iliyotolewa Julai mwaka huu imepingwa na walimu nchi nzima, kwani mbali ya kuwa ndogo sana imetolewa kwa upendeleo na walimu wanataka kujua ni kwa nini watumishi wengine waongezwe kwa asilimia kumi na walimu asilimia 6.35.

No comments:

Post a Comment