Pages
Simplfy language
thanx
Saturday, September 13, 2014
DUH!!!! BOKO HARAM ZAIDI YA 100 WAUWAWA..
Zaidi ya wanamgambo 100 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram nchini Nigeria wameuawa na jeshi la nchi hiyo katika mapigano makali yaliyojiri kati ya pande mbili jana Ijumaa. Kwa mujibu wa jeshi la Nigeria, mapigano hayo yalijiri katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na kulitia hasara kubwa kundi hilo ambapo mbali na idadi hiyo kuuawa, makumi ya wengine wamejeruhiwa. Inaelezwa kuwa wanachama wa kundi hilo
walikuwa wanakusudia kuudhibiti mji wa Konduga, ulio kilometa 35 kutoka jimbo la Maiduguri ambapo hata hivyo juhudi hizo ziliishia patupu baada ya kukabiliana na mashambulizi makali ya jeshi la nchi hiyo suala lililowafanya wapiganaji wa Boko Haram kukimbia. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Nigeria, wanachama wa kundi hilo waliamua kukimbia baada ya masaa matatu ya mapigano.
Mji wa Konduga ulishambuliwa mapema mwaka huu na wanachama wa kundi hilo, na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 5o sambamba na kuteketezwa kwa moto makumi ya nyumba za mji huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment