Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Tuesday, July 8, 2014
Shambulio la bomu Arusha wakamatwa wawili......
Watu wawili wamekamatwa na Polisi wakihusishwa na shambulio la bomu lililotokea kwenye mgahawa wa 'Vama Traditional Indian cuisine' jijini Arusha Kaskazini mwa Tanzania.
Shambulizi hilo lilitokea siku ya jumatatu saa nne usiku.
Watu wasiojulikana walirusha bomu ndani ya mgahawa kupitia mlangoni ambapo watu wanane wamejeruhiwa mmoja kati yao akiwa na majeraha makubwa.
Aidha,katika matukio mengine, jumla ya Watu 20 wanazuiliwa na Polisi wakiwemo watu sita wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bomu uliotokea mkoani Arusha juma lililopita nyumbani kwa Kiongozi wa dini Sheikh Sudi Ally Sudi na kujeruhi watu wawili.
Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment