Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Monday, July 7, 2014
MZAZI AMCHOMA KISU MWALIMU MBELE YA MWANAE..
Mwanamke mmoja ameripotiwa kumchoma kisu na kumuua mwalimu wa kike wa shule ya msingi mbele ya wanafunzi wake katika mji wa Albi ulio kusini mwa Ufaransa.
Muendesha Mashtaka wa Albi, Claude Derens ameiambia AFP kuwa tukio hilo limetokea jana (July 4) majira ya asubuhi kwa saa za Ufaransa na kwamba uchunguzi unafanyika ili kubaini sababu zilizopelekea mwanamke huyo kufanya tukio hilo la kikatili.
“Mama huyo alionekana akiwa na kisu na akamchoma mwalimu wa kike mwenye umri wa miaka 34 mbele ya wanafunzi wake, sababu itafahamika baada ya uchunguzi kukamilika.”
Claude Derens aliiambia AFP.
Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo, rais wa Ufaransa Francois Hollande alimtuma waziri wa elimu, Benoit Hamon haraka katika shule hiyo ili kuhakikisha anachukua hatua kama mwakilishi wa serikali.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment