Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Tuesday, July 8, 2014
MAMA AKIRI KUWAUWA WATOTO WAKE..
Baba ya waoto hao alikuwa amesafiri kwenda Afrika Kusini
Mama mmoja amekiri kuwaua watoto wake watatu kwa sababu ya ulemavu wao.
Tania Clarence,mwenye umri wa miaka arobaini na miwili alikiri kosa hilo la kuwaua watoto wake watatu wakiwemo vijana pacha wa miaka mitatu na msichana mmoja mwenye umri wa miaka minne kwa misingi kuwa wanawe walikuwa walemavu mno.
Mama huyo ambaye ametoka eneo la New Malden kusini Magharibi mwa London,alikana kufanya mauaji hayo. Watoto hao ambao walikuwa na ugonjwa wa uti wa mgongo,walipatikana nyumbani kwao tarehe 22 Aprili mwaka huu.Baba ya watoto hao alikuwa ameenda Afrika Kusini wakati wa mauaji hayo.
Ugonjwa huo wa kimaumbile husababisha watoto kuwa na uwezo mdogo sana wa kusongesha mwili na pia huwa hawaishi kwa mda mrefu.
Mwanamke huyo alitibiwa kwa majereha aliyoyapata kwa kujikata na baadaye kushitakiwa tarehe ishirini na nne Aprili.
Alizuiliwa katika hospitali ya matibabu ya akili na tarehe ya kesi kupangwa siku ya ishirini na tatu Februari mwaka ujao katika korti iyo hiyo.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment