Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Thursday, June 5, 2014
SKETI FUPI YAMPELEKA MAHAKAMANI......
Koplo wa Kitengo cha Traffiki aliyepigwa picha akiwa amevalia sketi iliyomabana makalio amelazimika kukimbilia mahakamani kuokoa kazi yake.
Linda Okello alikimbilia Mahakamani Baada ya wakubwa wake kutaka kumchukulia hatua ya kinidhamu wakidai alikosa nidhamu ya kazi alipovalia sketi iliyoonesha umbo lake akiwa kazini
Dada huyo aliyezua mjadala kote duniani kuhusu wanawake waliojaliwa makalio makubwa na kama wanabaguliwa kutokana na maumbile yao amemshtaki Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya miongoni mwa tume inayosimamia polisi nchini humo.Kinyume na kanuni za idara ya polisi ya mwaka wa 2011.
Koplo Linda anasema kuwa Afisa mkuu wa wilaya ya kiambu Stephen Ngetich hata hakuwepo katika eneo la tukio lakini ndiye aliyemshmtaki.
Linda alipigwa picha akilinda usalama katika mashindano ya mbio za magari ya Kiambu na picha hiyo ikaenea sana katika mitandao ya kijamii kuhusiano na urefu wake na pia makalio na umbo lake .
Makalio makubwa yamtia Koplo wa polisi matatani
Sasa koplo huyo anaitaka mahakama ifutilie mbali kesi ilyoko dhidi yake akisema,kuwa anahisi ataonewa na wakubwa wake kutokana na majaliwa yake .
Aidha koplo huyo huyo anasema kuwa japo alipewa Suruali ndefu mbili iliasiivae tena sketi hiyo yake ,Koplo anadai kuwa bosi wake hakuwahi kumkaripia kwa kuivalia na kuwa madai dhidi yake yanashinikizwa tu na watu waliovutiwa na mjadala katika mitandao ya kijamii.
Alipigwa picha na mwanahabari mmoja wa gazeti moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake kazini mjini Kiambu.
Lakini punde si punde picha hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya kijamii na baadhi wakiikejeli.
Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya kumbana.
Nini Kauli yako?
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment