 Mume wa Farzana Parveen ambaeni mwanamke mjamzito wa Pakistan 
aliepigwa mawe hadi kufa kutokana na kuamua kuolewa na Mwanaume 
anaempenda kinyume na pendekezo la familia la kutaka aolewe na mwanaume 
wanaemtaka wao, amekiri kufanya mauaji ya mke wa kwanza kabla ya Farzana
 na kusema alifanya hivyo ili aweze kufunga ndoa na Parveen
Mume wa Farzana Parveen ambaeni mwanamke mjamzito wa Pakistan 
aliepigwa mawe hadi kufa kutokana na kuamua kuolewa na Mwanaume 
anaempenda kinyume na pendekezo la familia la kutaka aolewe na mwanaume 
wanaemtaka wao, amekiri kufanya mauaji ya mke wa kwanza kabla ya Farzana
 na kusema alifanya hivyo ili aweze kufunga ndoa na ParveenMwanaume huyo Mohammad Iqbal amesema alitaka kuwasilisha maombi yake kwa Parveen hivyo aliamua kumuua mke wake kwanza ambapo mamlaka za nchini Pakistan zimesema ni kweli Mwanamke huyo wa kwanza aliuwawa miaka sita iliyopita.
Baaday a mauaji Iqbal alikamatwa na polisi na baadae kuachiwa kwa dhamana kwasababu mtoto wake wa kiume alimsamehe kutokana na kitendo hicho.
Mtoto wake ambaye kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka 20, amethibitisha taarifa hizo na kusema baba yake alitumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani kutokana na mauji hayo.
Parveen ambae ndio mke wa pili baada ya wa kwanza kuuwawa, alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu na alipigwa mawe hadi kufa na kundi la watu wakiwemo kaka zake, baba yake mzazi na ndugu wa familia yake Mashariki mwa mji wa Lahore kwa sababu aliamua kuolewa na Mwanaume ambae familia yake haikua inamtaka.
Tayari waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif amemtaka waziri wa Jimbo hilo kuwasilisha maelezo juu ya tukio hilo la Mwanamke huyu kuuwawa na ujauzito wake.
Hutaki kupitwa na stori kubwa kama hizi? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza
 
 
 
No comments:
Post a Comment