Jeshi
 la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu 34 wakazi wa Mji mdogo wa 
Kibaigwa Kata ya Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma kwa makosa ya 
kufanya fujo na kuharibu mali tukio lililotokea tarehe 05/05/2014 majira
 ya saa 13:30Hrs
.
Kamanada
 wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID 
MISIME – SACP amesema Vijana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya miatatu 
wakishirikiana na Wabeba mizigo wa Soko Kuu la Mazao la Kibaigwa, 
walifanya maandamano bila kibali na kung’oa bango la Halmashauri ya 
Wilaya ya Kongwa lenya tangazo la kutoruhusu wafanyabiashara kuingiza 
mazao sokoni bila kulipa ushuru uliowekwa kwa mujibu wa sheria. 
Kamanda MISIME amesema chanzo cha vurugu hizo ni wabeba mizigo wa soko la mazao kibaigwa kupinga kitendo cha Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuweka tangazo la kutoza ushuru wa mazao sokoni hapo wakidai kwamba linawakosesha kufanya kazi zao kwani wateja wanashindwa kuingiza mazao sokoni na wao kukosa kazi.
 

 
 
No comments:
Post a Comment