Mtumishi wa idara ya Afya katika halmashauri ya mji wa kahama, Mkoani
 Shinyanga, Jeremiah Munuo (50) amekutwa amefariki dunia katika nyumba 
moja ya kulala wageni mjini Kahama.
Taarifa kutoka jeshi la polisi wilayani humo zimesema kwamba Tukio 
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika nyumba hiyo iitwayo KK Lodge 
iliyopo jirani na ofisi za Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Taarifa zimesema watumishi wenzake walikwenda kumuona leo majira ya 
saa 6 mchana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa muda mrefu.
Jesh la polisi wilayani Kahama limefika katika eneo la tukio na 
kumkuta marehemu Munuo ambaye alikuwa na miezi 3 tu tangu ahamishiwe 
katika halmashauri hiyo akiwa na Fedha taslimu shilingi 596,000 na simu 
nne za mkononi.
Mwili wa marehemu Munuo umepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya hiyo na uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea.
 


 
 
No comments:
Post a Comment