Kampuni kubwa ya kutengeza magari nchini  Marekani imeagiza  magari milioni 1.4 yarejeshwe 
kutokana na hitilafu ya usukani.
Takriban magari milioni 1.1 yaliyoundwa kwa 
mtindo wa kispoti yaliyokuwa yameuzwa Marekani Kaskazini yametakiwa 
kurejeshwa  kwani huenda yana hitilafu kwenye usukani.kutokana na hitilafu ya usukani.
Vilevile magari mengine 200,000 yenye muundo wa Taurus yaliyoundwa kati ya mwaka wa 2010 na 2014 huenda yakakumbwa na tatizo ya kushika kutu kwa haraka.
Matukio kama hayo yaliyofanyika majuzi huenda yakaifanya kampuni hiyo kuvunja rekodi ya kutaka magari mengi zaidi yarejeshwe katika kipindi cha mwaka mmoja.
Urejesho huo umetokea wakati sakata ya usalama inawakumba wapinzani wakuu wa kampuni ya hiyo , General Motors (GM).
GM ililaumiwa kwa kutotoa ilani za kiusalama kwamba baadhi ya magari yake hata baada ya kubaini kuwa magari hayo yanazima ghafla.
Dosari hiyo imehusishwa na vifo 13, ingawa wasanifu wa Marekani wanaamini kuwa idadi hiyo itaongezeka.
Pindi tangazo hilo lilipofanywa, kampuni za kutengeneza magari hayo pamoja na wasanifu wa Marekani wameongeza juhudi za kurejesha magari ambayo yanapatikana kuwa na dosari
 


 
 
No comments:
Post a Comment