Pages
Simplfy language
thanx
Tuesday, May 6, 2014
BUNGE SASA LAWAKA MOTO WABUNGE WATAKA RAIS AJIUZULU..
Wabunge wametoa wito wa kujiuzulu Rais Hassan Sheikh Mohamud wa somalia wakimtuhumu kwamba, ameshindwa kuiongoza nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Taarifa zaidi kutoka Somalia zinasema kuwa, Wabunge 135 kati ya 275 wa Bunge la nchi hiyo wanataka Rais Hassan Sheikh Mohamud aachie ngazi.
Wabunge hao walitoa mwito huo jana baada ya mkutano wao uliofanyika katika hoteli moja mjini
Mogadishu mji mkuu wa nchi hiyo. Katika wito wao huo, Wabunge hao wanasema kwamba, tangu Rais Hassan Sheikh Mohamud achukue madaraka ya nchi hiyo Septemba mwaka 2012 hajafanikiwa kabisa katika kuendesha masuala ya nchi. Wabunge hao wamesisitiza kwamba, kama Rais huyo hatajiuzulu basi watataka kupigwe kura Bungeni ya kutokuwa na imani naye. Rais Hassan Sheikh Mohamud anatuhumiwa kwamba, ameshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kwamba, hana mpango wa kisiasa wa kuitisha uchaguzi wa Rais mwaka 2016. Kwa mujibu wa Katiba ya Somalia, Wabunge watakuwa tu na uwezo wa kumsaili Bungeni Rais baada ya jambo hilo kuchunguzwa na na kupasishwa na Mahakama ya Katiba. Somalia ni miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani ambayo mbali na kukumbwa na ukame mkubwa ina matatizo mengine chungu nzima likiwemo la ukosefu wa usalama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment