Pages
Simplfy language
thanx
Friday, April 4, 2014
EBOLA NI TISHIO..
Viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Kongo wamechukua tahadhari kubwa ya kukabiliana na virusi vya homa ya ebola.
KUMRADHI KWA PICHA HII MSOMAJI WETU,,,,,,WA newinfotz.blogspot.com
Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kongo imetangaza leo mjini Brazzaville kwamba, nchi hiyo imechukua hatua
za dharura na kuweka indhari kubwa kwenye mipaka ya nchi hiyo baada ya kusambaa homa ya ebola katika baadhi ya nchi za Magharibi mwa Afrika. Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kongo imetangaza kuwa, moja ya hatua hizo ni kukaguliwa afya za wasafiri wote wanaoingia nchini humo wakitokea nchi za Magharibi mwa Afrika na hasa Guinea, kwani kuna uwezekano kwa wasafiri hao kubeba virusi vya ugonjwa huo hatari. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwaka 2005, Jamhuri ya Kongo ilikumbwa na homa ya ebola na kusababisha makumi ya watu kufariki dunia. Tokea homa ya ebola ilipoanza kushuhudiwa nchini Guinea katika wiki za hivi karibuni na kusambaa katika nchi jirani, nchi nyingine za Kiafrika zimeanza kuchukua hatua za tahadhari za kukabiliana na homa hiyo. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa juzi tarehe Pili Aprili, watu wasiopungua 83 wameshafariki dunia na wengine wasiopungua 127 wanashukiwa kukumbwa na homa hiyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment