Pages
Home
Kitaifa
Kimataifa
Michezo
Burudani
Makala
Usilolijua
Leo katika historia
Picha
Teknolojia
Afya
Simplfy language
thanx
Friday, March 28, 2014
LEO KATIKA HISTORIA
Ijumaa, Machi 28, 2014
Leo ni Ijumaa tarehe 26 Jamadil Awwal 1435 Hijria inayosadifiana na Machi 28, 2014
.
Miaka 146 iliyopita katika siku kama ya leo alizaliwa mwandishi mashuhuri wa Russia Maksim Gorky. Gorky alilazimika kusoma na wakati huohuo akifanya kazi ili kuweza kukidhia mahitaji yake ya maisha kutokana na umaskini mkubwa uliokuwa ukimkabili. Alianza kuandika riwaya haraka sana na kufanikiwa kuchapisha riwaya yake ya kwanza katika gazeti la Tbilisi wakati alipokuwa akifanya kazi katika sekta ya reli. Miaka miwili baadaye mwandishi Gorky alipata mafanikio makubwa ambapo alichapisha riwaya yake katika kitabu na taratibu akaanza kuingia katika safu ya waandishi wakubwa na mashuhuri duniani.
Siku kama hii ya leo miaka 75 iliyopita baada ya kupita karibu miaka miwili na nusu tangu kujiri vita vya ndani huko Uhispania, wapigania usultani chini ya uongozi wa Jenerali Francisco Franco waliwashinda Warepublican na kudhibiti Madrid, mji mkuu wa nchi hiyo. Machafuko yalitokea huko Uhispania wakati Alphonso wa 13 mfalme beberu wa nchi hiyo alipolazimika kujiuzulu kufuatia mashinikizo ya Warebuplican na baadaye mfumo wa jamhuri ukaasisiwa huko Uhispania.
Na Siku kama ya leo miaka 1154 iliyopita, alifariki dunia Abu Hanifah Ahmad bin Daud Dinawari. Dinawari alibobea katika elimu za nahau, lugha, fasihi, hesabu, nujumu na balagha. Mbali na kutabahari katika elimu mbalimbali za kidini, Dinawari alikuwa bingwa katika elimu ya falsafa. Miongoni mwa vitabu vya mwanazuoni huyo ni pamoja na vitabu vya “al-Shi’ri wa al-Shuaraa”, “al-Nabat”, “al-Jabru wal-Muqaabalah” na “al-Buldan.”
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment